
Zoezi la uandikishaji daftari la kudumu la wapigakura mkoani Morogoro limeanza rasmi huku likigubikwa na changamoto lukuki zikiwemo wananchi kulalamikia kuamka saa kumi usiku huku mashine zikigoma kufanya kazi na kusababisha usumbufu kwa wananchi hasa wazee na wajawazito kukata tamaa ya kujiandikisha.
ITV imtembelea vituo mbalimbali vikiwemo kituo cha kata ya Bondwa mkoani Morogoro na kukuta idadi kubwa ya wananchi wakiwemo wajawazito na wazee ambapo wananchi wamesema mashine zinatumia zaidi ya nusu saa kuandikisha mtu mmoja kutokana na mashine hizo kushindwa kufanya kazi kama inavyotakiwa ambapo wameiomba tume ya uchaguzi kuongeza muda wa kutosha kujiandikisha ili kila mwananchi apate haki yake ya kupiga kura.
Kwa upande wake fundi anayeshughulikia ukarabati wa mashine hizo kutoka tume ya uchaguzi amekiri mashine hizo kushindwa kufanya kazi kwa muda lakini kufikia muda wa mchana mashine zimerekebishwa na kutoka na wingi wa wananchi waliojitokeza kwenye zoezi hilo wamelazimika kuongeza mashine ili kupunguza kero ya foleni kwa wanchi

0 comments:
Post a Comment