
Akichangia maoni ya hotuba ya bajeti ya serikali ya mwaka 2015/16,
mbunge wa viti maalum, Mhe Esther Matiko amesema barabara hiyo haina
maeneo ya watembea kwa miguu, pikipiki, na upana wa barabara hiyo
hauwezi kuruhusu malori mawili kupita kwa wakati mmoja na kusisitiza
inaufisadi wa hali ya juu, huku mbunge wa Singida Magharibi akiitaka
serikali kuhakikisha inafuatilia fedha katika benki ya Exim ili
kutekeleza mradi wa umeme wa upepo ulioanza takribani miaka saba
iliyopita.
Aidha, suala la ongezeko la tozo katika mafuta limechukua nafasi
kubwa ya miongoni mwa wabunge katika mjadala wa hotuba ya bajeti kwa
siku ya tano mfululizo ambapo mbunge wameendelea kuilalamikia serikali
kwa kuweka tozo katika mafuta hususani ya taa na kuhacha vinywaji baridi
na vikali ambavyo simahitaji ya lazima ukilinganisha na umuhimu wa
mafuta ya taa, huku wengine wakisisitiza lazima wananchi wa sasa waumie
kwa faida ya vizazi vijavyo.
Aidha bunge limeitimisha mjadala wa hituba ya bajeti ya serikali
kwa mwaka wa fedha 2015/16 ambapo siku ya jumatatu mawaziri mbalimbali
wataanza kujibu hoja zilizokuwa zikitolewa na wabunge kwa takribani siku
tano za mjadala wa hituba ya bajeti ya serikali ya shilingi trillioni
22.495 kwa mwaka wa fedha 2015/16.

0 comments:
Post a Comment